Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: George Kordahi amesisitiza kuwa, hatua yake ya kujiuzulu haina maana ya kufikia tamati majukumu yake ya kisiasa bali ndio kwanza yameanza.
Akizungumza jana Jumatano Waziri wa zamani wa Habari wa Lebanon amesema kuwa, baadhi ya watu wanadhani kwamba, wanaweza kubana maisha yangu ya kisiasa, katika hali ambayo, matukio yaliyotokea kwa namna fulani yamenisukuma upande wa medani ya kisiasa.
Matamashi hayo ameyatoa siku chache baada ya hivi karibuni kunukuliwa akisema kuwa, muda si mrefu ukweli na uwongo utafahamika na kwamba, kujiuzulu kwake hakuwezi kudhamini kurejea uhusiano baina ya Lebanon na Saudi Arabia.
Kabla hajateuliwa waziri, Kordahi aliwahi kuikosoa vikali Saudi Arabia kwa kuanzisha vita dhidi ya Yemen na kusema vita hivyo haviwezi kuendelea milele. Katika mahojiano ya Mwezi Agosti ambayo yalirushwa hewani Oktoba baada ya kuteuliwa waziri, Kordahi alisema vita dhidi ya Yemen ni uvamizi ambao unatekelezwa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Alisema vita hivyo ni vya kipuuzi na vinapaswa kusitishwa huku akisema anapinga vita baina ya mataifa ya Kiarabu.
Matamshi ya Kordahi yaliikera sana Saudia ambayo ilivunja uhusiano wake na Lebanon na hatua hiyo ikafuatwa na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain na Kuwait. Baadaye George Kordahi alijiuzulu ili kupunguza mgogoro wa nchi yake na Saudi Arabia baada ya kauli yake ya kukosoa vita vya Saudia dhidi ya Yemen.
342/